Saa Heri Ya Maombi//Sweet Hour of Prayer//NZK 135

Saa Heri Ya Maombi//Sweet Hour of Prayer//NZK 135

[1] Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi, Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu. Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona, Mashaka tumeshinda, wakati wa saa tamu. [2] Saa heri ya maombi, twapeleka dhiki zetu Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja. Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake, Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu. [3] Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia, Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo. Yesu atatusikia, tutamtafuta daima, Na tutakapokutana tutamwona - saa tamu!